Kulinda mazingira
Utajiri wa mazingira unavyobadilika na tunavyotumia arthi © Chris Heward/GWCT
Ulinzi na uthibiti wa maeneo asili na michakato ni muhimu wakati shinikizo kuhusu mazingira ni nzuri zaidi. Maeneo ya kukimbilia ni muhimu kwa viumbe vinavyopotea kwa urahisisi katika mfumo wa Ikolojia, ili kuwe na kuwepo kwa urejesho. Utajiri wa viumbe katika sehemu safi sana zilizobaki za nchi za tropiki tayari uko juu na unawezwa kuhifadhiwa bila haja ya urejesho. Zaidi ya sehemu kama hizi, umuhimu wa kuhifadhi viumbena mfumo wao wa ikolojia ni uendelezaji wa uhifadhi, ambapo sehemu za ulinzi huwekwa mipaka na kuhusishwa na maeneo au mikanda ya makao asili iliyo na matumizi yaliyopunguzwa na binadamu, kutengeneza urembo. Iwapo mazingira yaliyohifadhiwa yatakuwa visiwa katika bahari ya utumizi mkubwa, yanahatarisha kufurika kwa vichafuzi au kupoteza maji na kuna uwezo mdogo wa kubakisha idadi ya viumbe nadra. Kuwa na sehemu pia kunawezesha jamii kushughulika sanakatika uhifadhi mashinani kuliko kulipia usafiri na kuingia katika maeneo ya mazingira tajiri. Katika Namibia, Afrika Kusini na Zimbabwe, ardhi zaidi na idadi kubwa ya wanyama pori huthibitiwa nje ya mbuga za kitaifa kuliko ndani yake, kupitia uwindaji na kuwatazama. Maeneo kama haya ni sahihi haswa kwa viumbe ambavyo jamii za mashinani huvikubali iwapo tu uharibifu wowote vinavyoweza kusababisha unaweza kuondolewa na manufaa kutoka kwa uwindaji au matumizi mengine. Kinacholipa, kinakubalika.
Kurejesha na kuimarisha mazingira
Kurejesha mikoko ya pwani, picha © Marco Quesada
Ingawa ulinzi fulani umefauli kwa kama 15% ya ardhi ulimwenguni, mfumo wa ikolojia unaotumika na binadamu unaendelea kushushwa na viumbe vinapotezwa kwa wingi mashinani kupitia juhudi za juu za binadamu za kupata chakula na nyenzo. Shida ya miundombinu ya kibinaadamu, kama vile barabara, mabwawa, nyaya za umeme, na mashine zinazotegemea upepo zinaweza kupunguzwa iwapo maarifa mwafaka yatatumika. Kama kupoteza makao ni shida, mabadiliko madogo sana katika usimamizi wa ardhi, ambao wakati mwingine kwa hakika hunufaisha ukulima, upandaji miti na utunzaji bustani, unaweza kuwa na athari kubwa kwa utajiri wa mazingira. Masanduku ya viota, 'benki ya wadudu', vipande vya ardhi vya kutunza ardhi na matumizi mseto ya ardhi yote ni mifano mizuri. Kazi nyingi zaidi inahitajika kwa huu 'upatanisho wa ikolojia' na ujumuishaji bila tashwishwi katika uthibiti wa ardhi ( ikiwemo majiji) na miundombinu.
Iwapo uvunaji wa vyakula mwitu utaondoka kwa viwango vya hapo awali vya matumizi mazuri, haswa kwa nyama ya masoko katika miji inayokuwa, ni mhimu kukubaliana njia za utunzaji na jamii, kulingana na sayansi ya kisasa na ujuzi wa kitamaduni. Kumiliki kwingi kwa uhifadhi wa kijamii umecheleweshwa na jamii nyingi ambazo hazijataka ugatuzi wa majukumu kwa uthibiti wa mfumo wa ikolojia kufikia viwango mwafaka vya chini ('kushughulikia mfumo wa ikolojia') na kupitia kwa imani kuwa ni vizuri zaidi kwa maendeleo kupingwa kuliko uthibiti na urejesho kutumiwa kufidia athari za kibinaadamu. Ingawa urejesho umetajwa sana kwa mikakati rasmi, utekelezaji ni mbaya. Serikali na mashirika mengine yanahitaji kushirikiana vizuri zaidi kwa urejesho , pamoja na jamii za mashinani na jamii za wote wanaovutiwa na ardhi na viumbe vya mwituni. Jamii zilizovutiwa zinaweza kuwa na nafasi spesheli, kama vile wapendao ndege wa kipanga wanapounda nyaya salama za umeme na wapenda ndege wanapotafuta kuweka kwa makini mashamba ya upepo.
Mifumo ya Ikolojia ya mijini.
Utofauti wa mimea unahimiza utofauti wa wanyama pia © Jamesteohart/Shutterstock
Kuhifadhi na kujenga tena utajiri wa mazingira unahitaji kujumuisha si mashinani tu lakini pia sehemu za mijini, kwa sababu kila mtu hutegemea mazingira kwa chakula, maji freshi, hewa tunayoweza kupumua na hali ya mazingira thabiti. Bustani, za nyumbani na za umma, "mapafu ya kijani" na 'mikufu ya zumaridi' kuzuia uchafuzi mijini inaweza yote kuleta manufaa, kwa sababu usimamizi wa huduma za binadamu na maisha mengine unahitajika kila pahali. Zaidi, watu wanaoishi mijini hurudi mashambani, na wanahitaji kuelewa mazingira iwapo watachangia kimanufaa kwa jamii za mashambani.